1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haipo tayari kukubali madai ya nchi za Magharibi

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVU2

Kwa mara nyingine tena,Iran imesema kuwa haipo tayari kubadili msimamo wake kuhusu mradi wake wa kinyuklia.Msuluhishi wa Iran,Saeed Jalili baada ya kukutana na mkuu wa sera za Umoja wa Ulaya,Javier Solana mjini London alisema,madai ya nchi za Magharibi kuwa Iran isite kurutubisha madini ya uranium hayakubaliki.

Kwa upande mwingine,Solana alisema kuwa amevunjika moyo,kwani baada ya mazungumzo ya saa tano pamoja na Jalili alitegemea mengi zaidi.Leo hii,nchi tano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani,zinakutana mji mkuu wa Ufaransa,Paris kujadili hatua ya kuchukuliwa kuhusika na mgogoro wa Iran.