1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haitakaa mezani na Umoja wa Ulaya

6 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DJFx

TEHRAN

Rais wa jamhuri ya kiislamu ya Iran Mahmoud AhmediNejad amesema serikali yake haiwezi kukaa kwenye meza ya mazungumzo mapya na Umoja wa Ulaya kuhusu mpango wake wa Kinuklia unaotiliwa shaka na nchi hizo pamoja na Marekani.

Badala yake rais huyo wa Iran amesema katika siku za baadae nchi yake itafanya mazungumzo na shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Kinuklia IAEA.Matashi hayo yanakuja siku tatu baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Iran baada ya taifa hilo kuktaaa kukomesha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Rais AhmedNejed amelitaja baraza hilo la usalama la Umoja wa mataifa kuwa ni chombo kinachotumiwa kisiasa na Marekani kuikandamiza Iran.Jumatatu iliyopita muda mfupi baada ya kupitishwa kwa azimio hilo la kuiwekea Iran Vikwazo nchi nyingi zenye nguvu zilimtaka mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana kuanzisha tena mazungumzo na mjumbe wa Iran anayehusika na suala hilo.Nchi nyingi za Magharibi zinahofia kwamba Iran inataka kutengeneza silaha za kinuklia wakati Tehran inasisitiza kwamba mpango wake ni kwa ajili ya matumizi salama kwa taifa lake.