1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran inashikilia haki yake ya kurutubisha Uranium

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBL

TEHERAN:

Iran imesisitiza haki yake ya kuwa na mradi wa kinyuklia unaozusha mvutano. Hata hivyo,Iran ipo tayari kuzungumza na nchi za Magharibi kuzihakikishia kuwa mradi wake wa kurutubisha madini ya Uranium ni wa matumizi ya amani tu.Hayo alitamka msemaji wa wizara ya nje,Mohamed Ali Hosseini.Mwanasiasa huyo ameendelea kusema, hata hivyo majadiliano hayo yafanywe bila ya kutolewa masharti yo yote yale ya awali .Msemaji huyo wa wizara ya nje amesisitiza pia kuwa Iran imejianda kikamilifu ili kujilinda pindi ikishambuliwa.