1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran katika Baraza la Usalama

23 Machi 2007

Dola 5 za kudumu katika baraza la Usalama la UM zataka kesho jumamosi kupitisha azimio lao dhidi ya Iran kutokana na ubishi wake juu ya mradi wa nuklia.

https://p.dw.com/p/CHHc

Dola kuu zanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zimefanya mageuzi madogo katika azimio lao jipya ili kukaza vikwazo dhidi ya Iran kutokana na mradi wake wa kinuklia.Zimeliweka tayari azimio hilo ili kupigiwa kura hapo kesho na Baraza la Usalama.

Baraza hilo la wanachama 15 lilikutana jana faraghani kuzingatia mageuzi katika azimio lililoafikiwa wiki iliopita na wanachama 5 wa kudumu wenye kura ya veto-Marekani,Uingereza,Ufaransa,Urusi na China pamoja na Ujerumani.

Azimio hili lisilo rasmi, linalozingatiwa sasa, litaipaga marufuku Iran, isiuze nje silaha na laitisha kuiwekea Iran kwa hiyari vikwazo vya biashara na kongeza orodha ya wakuu na makampuni ya Iran ambayo ni marufuku kusafiri na kufanya nayo biashara.

Dola zilizotunga azimio hili zilipinga mapendekezo ya Afrika Kusini ya kusimamishwa kwa siku 90 vijkwazo hivyo vya UM kabla kuanza kuruhusu mazungumzo ya kisiasa na Iran pamoja na kuiondolea marufuku ya silaha na vikwazo vya fedha.

Shauri la Indonesia na Qatar, kuingiza kifungu katika azimio hilo kinachoitisha eneo zima la Mashariki ya Kati kuwa huru na silaha za kinuklia na makombora ‘ lilikataliwa halkadhalika.

Dola zilizotunga azimio hili lakini, ziliafiki kuongeza lugha isemayo Shirika la Nguvu za Atomiki Ulimwenguni “ndilo dhamana duniani wa kuchunguza kutekelezwa na kuheshimiwa mapatano pamoja na kugeuza vifaa vya kinuklia kwa madhumuni ya kijeshi.”

Azimio hilo linakariri mpango wake wa kuipa Iran nafuu za kiuchumi na kidiplomasia zilizoahidiwa iran mwaka jana ikiwa ingeachana na kurutubisha madini ya uranium.

Rais wa Baraza la Usalama la UM kutoka Afrika Kusini Bw.Kumalo alikataa usemi kuwa mabadiliko yaliofanywa juu ya azimio hili ni ya urembo tu.

Kaimu muakilishi wa Marekani katika UM Alejandro Wolff alisema na ninamnukulu,

“Tumeridhia mageuzi yaliolingana na msingi na nia ya azimio ambalo linaegemea maazimio 2 yaliotangulia…”

Mjumbe wa Marekani akaongeza:

“Tumefurahi kwamba kura itapigwa juu ya azimio hili ambayo pengine itafanyika ijumaa jioni.”

Ikiwa itafanikiwa kulipigia kura azimio hilo leo jioni,basi rais wa Iran Mahmud Ahmadinejad hatakuwa na wsakati wa kwenda New York kama alivyoazimia kuzungumza na wajumbe.Dola za magharibi zinaazimia alao kesho jumamosi kwishalipitisha azimio hilo.

Hata hakuna wakati wa kuzingatia maombi ya mageuzi kwenye azimio hilo kutoka nchi zisizo-zanachama wa Baraza la Usalama la UM.

Mjumbe wa Uingereza katika UM,Jones Parry asema:

“Dai la kusimamisha vikwazo kwa siku 90 kwa mfano, hatukulikubali kwavile, hatukutaka kuitunza Iran kwa kuiregezea vikwazo …”

Kwa ufupi, hakuna hata dola moja kati ya hizo zilizotunga azimio hilo iliotaka au kuwa tayari kueleza kwanini wanaliharakisha kulipitisha haraka-haraka au kwanini kusubiri hadi jumatatu ni kukawilisha mambo.

Mjumbe wa Marekani Wolf:

“Kulikuwapo wakati wa kutosha sasa lakini wakati umefika wa kusonga mbele.”