1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kuwekewa vikwazo zaidi.

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVey

Vienna. Wawakilishi wa Marekani, Urusi , China , Ufaransa, Uingereza na Ujerumani wamekutana mjini Paris kujadili kuhusu mpango wa kinuklia wa Iran baada ya majadiliano ya mwisho kushindwa kuleta ufumbuzi. Duru za kidiplomasia nchini Ufaransa zimefichua kuwa wanachama hao watano wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani wamekubaliana kufanyakazi katika kutayarisha azimio jipya la vikwazo ili kuilazimisha Iran kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium. Amesema kuwa muswada utasambazwa wiki ijayo. Iran tayari imewekewa vikwazo mara mbili vya umoja wa mataifa, pamoja na vikwazo vya pekee vya Marekani kuhusiana na mzozo huo. Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic Mohammed El Baradei amesema kuwa shirika hilo haliwezi kuthibitisha kuwa mpango huo wa kinuklia wa Iran ni wa matumizi ya amani.