1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yafungua kinu cha pili cha kurutubisha Uranium

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyN

Teheran

Iran imetangaza rasmi imefungua kinu cha pili cha kurutubisha maadini ya Uranium.Gazeti la serikali Iran daily limesema hii leo gesi imeshaanza kuingia katika kinu hicho cha pili.Iran Daily limenukuu naibu mkurugenzi wa taasisi ya nguvu za kinuklea Mohammed Ghannad akisema maadini ya Uranium yatarutubishwa kwa kiwango cha asili mia tatu hadi tano.Katika kinu cha Natan kuna mitambo miwili ambayo kila mmoja una viuu 164 vya kurutubishia maadini ya Uranium.Wataalam wanasema Iran inahitaji vinu zaidi ya elfu kuweza kurutubisha maadini ya Uranium hadi kutengeneza bomu la kinuklea.