1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakosolewa kwa jaribio lake la kombora "Sejil 2 "

17 Desemba 2009

Iran imepeleka salamu kwa upinzani nchini na wakosoaji n'gambo.

https://p.dw.com/p/L65W
Ayatollah Ali Khamenei (Iran)Picha: AP

Watawala wa Iran wenye msimamo mkali, jana wliwatumia jana salamu zao kali mahasimu wao tangu nchini Iran hata n'gambo katika kambi ya magharibi, kwa kuwatishia kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi wa Upinzani nchini Iran na kwa kufanya jaribio la kombora kali zaidi linaloweza kufika Israel.Nchi za magharibi hazikupendezwa na hatua za Uongozi wa Iran na hasa kuhusu jaribio la kombora lake la "SEJIL 2".

Marekani imesema kwamba, kufyatuliwa jana kwa kombora "Sejil 2" na kuwa lina masafa ya kuifikia Israel na kambi za majeshi ya Marekani katika Ghuba,kunatoa maanani dai la Iran, kuwa ina nia njema za amani katika mradi wake wa kinuklia.Hii itaufanya ulimwengu kuzidi kuitilia shaka Iran na azma zake.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown ,alisema jaribio la kombora la Iran linapalilia haja ya kuwekewa hata vikwazo vikali zaidi juu ya mradi wake wa kinuklia.Ni mradi ambao kambi ya nchi za magharibi inadai unalenga kuunda bomu la nuklia wakati Iran, inashikilia kudai ni wa nishati ya kujipatia umeme.

Licha ya wasi wasi huo ulioelezwa na dola hizo 2 za magharibi, Marekani na Uingereza, msemaji wa vyombo vya habari wa wizara ya ulinzi ya Marekani-PENTAGON- mjini Washington Geoff Morrell, amesema jaribio hilo halikuleta matokeo mapya yoyote: Akaongeza na ninamnukulu,

"Sitafichua kwa urefu nini upelelezi wetu umegundua ,mbali na kusema hakuna kitu zaidi ambacho ni tofauti na kile tulichokiona zamani."

Wachambuzi wanadai kwamba, mchafuko wa kisiasa nchini Iran tangu ule uchaguzi wa rais wa kutatanisha hapo juni,mwaka huu umetatanisha zaidi ufumbuzi wa mradi wa nuklia wa Iran. Mvutano ndani ya Iran umeongezeka tangu wanafunzi wanaomuunga mkono mtetezi wa Upinzani, Mirhossein Mousavi, kupambana na vikosi vya usalama mjini Teheran wiki iliopita.

Serikali na vyombo vya habari vinavyo dhibitiwa na dola, imeutuhumu Upinzani nchini Iran, kumkashifu na kumbughudhi muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ,Ayatollah Ruhollah Khomeini, kwa kuichana picha yake wakati wa maandamano.Upinzani unakanusha lakini , kufanya hilo.Unadai serikali ina njama ya kukitumia kisa hicho kukandamiza Upinzani.

Jaribio la jana la kombora la "Sejil 2 " kwahivyo, limelaaniwa na nchi za magharibi.Waziri wa ulinzi wa Iran Ahmed Vahidi, amesema kombora hilo haliwezi kuteketezwa na silaha za kupambana na makombora kutokana na uwezo wake wa kupaa juu na kukwepa mitambo ya rada.

Afisa wa hadhi ya juu wa serikali ya rais Barack Obama, akikataa kutajwa jina, amenon'gona kwamba , wajumbe wa usoni wa kibalozi kutoka dola kuu zinazojadiliana na Iran juu ya mradi wake wa nuklia, watazamiwa kuwa na kikao pengine Ijuumaane ijayo kuzungumzia hatua gani ziichukulie Iran.Afisa huyo ametaja kwamba, wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UM pamoja na Ujerumani, wanaelekea kukaza zaidi vikwazo dhidi ya Iran ili kuilazimisha iachane na mradi wake wa nuklia.Iran ikionesha ukakamavu, imedai vikwazo haviiathri kitu.Afisa wake wa nishati alisema jana kwamba, vikwazo vya hivi karibuni vilivyo pendekezwa na wabunge wa Marekani, kuzuwia mafuta ya Iran kuuzwa n'gambo, hakutafanya kazi.

Mwandishi: Ramadhan Ali /RTRE

Mhariri:Abdul-Rahman