1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema haitazungumza na Trump mpaka aondoe vikwazo

Sekione Kitojo
27 Agosti 2019

Rais Hassan Rouhani wa Iran amebadilisha mwelekeo kuhusu uwezekano wa  mazungumzo na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, akisema, rais  huyo ni  lazima kwanza aondoe vikwazo alivyoiwekea Tehran.

https://p.dw.com/p/3OY6v
Iran, Teheran:  Präsident Hassan Rouhani und Außenminister Mohammad Javad Zarif
rais wa Iran Hassan RouhaniPicha: Reuters/Official President website

rais huyo wa  Iran amesema bila  hivyo mkutano  kati ya nchi hizo mbili utakuwa  tu fursa  ya kupiga picha za pamoja na  yeye  hayuko tayari kwa  hilo. 

Macron und Rohani | Kombo Bild
Rais wa Ufaransa (kushoto) Emmanuel Macron na rais wa Iran (kulia) Hassan Rouhani

Hatua  hiyo  ya  kubadilika  mwelekeo yamekuja  siku  moja  baada ya  Trump  kusema  jana  Jumatatu  kuwa  kuna  nafasi  nzuri viongozi  hao  wawili  wanaweza  kukutana  kuhusiana  na  mkwamo wao  wa  kinyuklia  baada  ya  hatua  ya  ghafla  ya  rais  wa Ufaransa  Emmanuel Macron  kuingilia  kati  wakati  wa   mkutano wa   mataifa  yenye utajiri  wa  viwanda wa  G7 , kujaribu kuzileta pamoja  Marekani  na  Iran  baada  ya  miongo  kadhaa  ya  mzozo.

"Bila ya  Marekani  kuondoa  vikwazo , hatutashuhudia maendeleo yoyote  yenye  manufaa," Rouhani alisema  katika  hotuba  aliyoitoa kwa  njia  ya  televisheni, leo , na  kuongeza  kuwa  Marekani "inashikilia  ufunguo" katika  kile  kitakachotokea  baadaye.

"Bila  ya  Marekani  kuondoa  vikwazo  na  kuacha  njia  potofu iliyochagua, hatuwezi  kushuhudia maendeleo  yoyote  ya  maana. Maendeleo  ya  maana  yako Washington."

G7-Gipfel in Frankreich| Symbolbild Streit unter Partnern
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto), na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia)Picha: picture-alliance/dpa/A. Harnik

Fursa ya mazungumzo

Mapema  jana  Jumatatu , Rouhani  alieleza  kuwapo  kwake  tayari kufanya  majadiliano  ili  kujitoa kutoka  katika  mzozo  huu  kufuatia Marekani  kujitoa  kutoka  katika  makubaliano  ya  kinyuklia.

"Iwapo nitafahamu  kwamba  kwenda  katika  mkutano  na kumtembelea  mtu  kutasaidia  maendeleo  ya  nchi  yangu  na kutatua  matatizo  ya  watu, sitaikosa  fursa  hiyo," alisema.  "Hata kama  uwezekano  wa  mafanikio  si  asilimia  90 lakini  asilimia  20 ama  10, ni  lazima  tusonge  mbele kuelekea fursa  hiyo. Hatupaswi kupoteza  fursa."

Rouhani  pia alimtetea  waziri  wake  wa  mambo  ya  kigeni , Mohammad Javad Zarif , dhidi  ya ukosoaji  kutoka  kwa  wenye misimamo  mikali  kuhusiana  na  ziara  yake  ya  kushitukiza  siku ya  Jumapili  katika  mji  wa  Ufaransa  wa  Biarritz, ambako viongozi wa  kundi  la  mataifa  saba  tajiri  walikuwa  wanakutana. Rohani alisema.

"Tunataka kutatua  matatizo lakini  kwa  kupitia  njia za  busara. Lakini  hatuhitaji  fursa za  kupigwa  picha. Iwapo  mtu  anataka kupigwa  picha  na  Hassan Rouhani , hilo  haliwezekani."

Iran, Teheran:  Präsident Hassan Rouhani und Außenminister Mohammad Javad Zarif
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif (kushoto) na rais wa Iran Hassan Rouhani (kulia)Picha: Reuters/Official President website

Televisheni  kwa  lugha  ya  Kiingereza  nchini  Iran  ya  Press TV ilitoa taarifa  isiyoeleweka  baadaye jana, ikikataa juhudi  za Macron.

Macron alisema  ana matumaini  Trump  na  Rouhani  wanaweza kukutana  katika  muda  wa  wiki kadhaa  zijazo  kwa  matumaini  ya kuyaokoa  makubaliano  ya  mwaka  2015  ya  kinyuklia  na  Tehran yaliyofikiwa  na  mataifa  yenye  nguvu  duniani, lakini  ambayo Marekani  iliamua  kujitoa  mwaka  jana.