1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema iko tayari kuzungumza lakini haitokoma kurutubisha Uranium

5 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EWq8

TEHRAN

Iran imesema iko tayari kuzungumza na nchi zenye nguvu duniani juu ya mpango wake wa kinuklia lakini bila ya kusimamisha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Matamshi hayo yametolewa na msemaji wa serikali Gholam hossein Elham siku moja baada ya hapo jana mjumbe wa Inchi hiyo katika suala la Nuklia Saedd Jalili kutoa jibu la nchi yake kuhusiana na mapendekezo ya vivutio vilivyotolewa na mataifa makubwa yenye nguvu duniani.

Mjumbe huyo wa Iran alisema kwamba nchi yake iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo na Marekani,Uingereza,Ufaransa,Urussi,China pamoja na Ujerumani kuzungumzia masuala yanayohusu pande zote mbili katika mpango wa Iran na mapendekezo yaliyotolewa na nchi hizo.Hatua hii mpya ya Iran imeonekana yenye kutoa matumaini katika kuutatua mzozo wa kinuklia wa nchi hiyo ambao nchi za magharibi unaamini unatumiwa kutengeneza silaha za Kinuklia.