1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema itaendelea na mradi wake wa Kinuklia liwalo liwe

4 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DHgT

TEHRAN

Iran imepinga azimio jipya la vikwazo dhidi yake lililoidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa mataifa hapo jana juu ya mpango wake wa Kinuklia.Iran imelitaja azimio hilo pamoja na vikwazo vya awali kwamba vinakiuka sheria ya kimataifa na kwamba zinachangia tu kuharibu uaminifu wa baraza hilo la wanachama 15. Iran imelishutumu baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kuwa kibaraka cha sera za nje za Marekani.Jana baraza hilo liliidhinisha duru ya tatu ya vikwazo dhidi ya Iran ili kuilazimisha isimamishe shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Indonesia ndio nchi pekee ambayo ilikataa kupigia kura azimio hilo hapo jana.Mjumbe wa nchi hiyo kwenye Umoja wa mataifa Marty Natalegawa alisema hatua hiyo sio nzuri kufikia sasa kwakuwa Iran imefanya juhudi zote na kushirikiana shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya kinuklia la IAEA kuonyesha mradi wake ni wa amani.....otone

Vikwazo hivyo ni pamoja na kuwazuia kusafiri maafisa wanaohusika na shughuli za kinuklia za Iran na mpango wa makombora halikadhalika idadi ya maafisa wa Iran ambao akaunti zao zitasimesimamishwa imeongeza.

Kwa mara ya kwanza azimo hilo linapiga marufuku biashara na Iran inayohusu bidhaa ambazo zinatumika katika masuala ya kiraia na kijeshi..Nchi za magharibi zinawasiwasi na Iran kwamba huneda inajaribu kutengeneza silaha za kinuklia lakini Iran imekuwa ikisisitiza kwamba mradi wake ni kwa ajili ya matumizi ya amani.Kabla ya kuidhinishwa vikwazo hivyo vipya hapo jana balozi wa Iran katika Umoja wa mataifa Mohammed Khazee aliliambia baraza la Umoja wa mataifa kwamba serikali ya nchi yake haitazingatia hatua hiyo ambayo sio ya halali dhidi ya mpango wake wa amani.