1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yatishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mataifa ya magharibi.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVei

Tehran.

Iran imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mataifa ya magharibi kuhusiana na vikwazo vya baraza la usalama la umoja wa mataifa vinavyohusu mpango wake wa kinuklia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Manouchehr Mottaki anaripotiwa kuwa ametuma barua kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ambapo anapinga azimio la vikwazo vya hivi karibuni kuwa ni kinyume cha sheria.

Iran inasisitiza kuwa haitatii vikwazo hivyo, ambavyo vilipitishwa March 3, na vina lengo la kuizuwia nchi hiyo kurutubisha madini ya uranium.