1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yawanyonga wafungwa 29 waliokutwa na makosa ya mauaji,ubakaji na biashara ya mihadarati

27 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/Ekky

TEHRAN

Iran leo imewanyonga wafungwa 29 waliohukumiwa kifo baada ya kukutikana na hatia ya kuhusika na mauaji,ubakaji,biashara ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine.

Mahakama ya Iran imethibitisha mauaji hayo ya wafungwa hao ambayo yamefanywa kwa wakati mmoja katika jela ya Evin kaskazini mwa mji mkuu Tehran.

Kunyongwa wafungwa hao kunaifikisha idadi ya watu walionyangwa nchini humo mwaka huu kuwa watu 100.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Armnesty International limesema Iran ni ya pili baada ya China katika nchi zinazoongoza kwa unyongaji wafungwa katika mwaka 2007 ambapo iliwanyonga wafungwa 314.