1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISIOLO:61 wajeruhiwa baada ya basi kupinduka

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9f

Takriban watu 15 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kaskazini mwa Kenya baada ya basi moja kupata ajali jana usiku.Kulingana na mkuu wa huduma za afya wa Wilaya Bwana Ahmed Omar watu 61 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika hospitali za eneo la Modagashe.Watu wawili wanaripotiwa kuwa mahututi na wengine hawako hatarini.

Basi hilo lililojaa abiria limepinduka na kubingiria zaidi ya mara tatu kaskazini mashariki mwa Kenya.Ajali hiyo ilitokea jana usiku mji.Polisi walilazimika kutumia tingatinga ili kulisogeza basi hilo waweze kuoka abiria walionasa.Kulingana na Antony Kibuchi mkuu wa polisi katika mkoa wa kaskazini,idadi ya abiria katika basi hilo ilipindukia.