1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Benazir Bhutto kutoshitakiwa.

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKg

Maafisa wa ngazi za juu wa Pakistan wamekubaliana kumpa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo aliyekuwa akiishi uhamishoni Benazir Bhutto msamaha wa kutokushitakiwa kutokana na kesi ya ujali rushwa dhidi yake.

Waziri wa reli Sheikh Rashid Ahmad amesema kuwa uamuzi huo umekuja kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri pamoja na maafisa wengine mjini Islamabad. Mwakilishi wa wizara ya habari Tariq Azim amesema kuwa taarifa zaidi zitapatikana baada ya siku kadha.

Kwa nia ya kutaka maridhiano ya kitaifa , tumeamua kufuta mashtaka yote na kwa hiyo mtasikia taarifa rasmi kuhusiana na hayo katika muda wa siku moja ama mbili zijazo.

Bhutto amekuwa na mazungumzo kwa wiki kadha na rais Pervez Musharraf juu ya uwezekano wa makubaliano ya kugawana madaraka.Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya luteni jenerali Ashfaq Pervez Kiani kuteuliwa kuchukua nafasi ya rais Pervez Musharraf kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo. Kiani atachukua wadhifa huo iwapo generali Musharraf atashinda uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi. Musharraf ameahidi kujiuzulu kuwa mkuu wa majeshi iwapo atashinda muda mwingine wa miaka mitano madarakani. Wakati huo huo , kiasi cha wabunge 80 wa upinzani nchini Pakistan wamejiuzulu kutoka katika bunge wakipinga dhidi ya nia ya Musharraf kutaka kugombea tena kiti cha urais.