1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Bhutto amtaka Musharraf kujiuzulu.

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1Z

Kiongozi wa upinzani wa Pakistan na waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto amedai kujiuzulu kwa rais jenerali Pervez Musharraf . Bhutto hivi sasa yuko chini ya kizuizi nyumbani kwake kwa mara ya pili kumzuwia kuongoza maandamano ya kilometa 300 kutoka Lahore kwenda Islamabad kupinga dhidi ya amri ya hali ya hatari iliyowekwa na jenerali Musharraf siku 11 zilizopita. Hivi sasa amesema kuwa anajadiliana na Nawaz Sharif , kiongozi aliyeondolewa madarakani akiwa kama waziri mkuu katika mapinduzi ya mwaka 1999 na Musharraf. Marekani imesema kuwa naibu waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo John Negroponte, atakwenda nchini Pakistan baadaye wiki hii kumtaka jenerali Musharraf kuondoa amri ya hali ya hatari na kuitisha uchaguzi huru.