1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Blair azuru Pakistan.

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrU

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amewasili nchini Pakistan kwa mazungumzo na rais Pervez Musharaff na viongozi wengine.

Mazungumzo yao yanatarajiwa kulenga katika mapambano dhidi ya ugaidi, hali nchini Afghanistan na uimarishaji wa mahusiano baina ya nchi hizo.

Blair anatarajiwa kutangaza ongezeko la msaada wa Uingereza kwa pakistan katika muda wa miaka mitatu ijayo hadi kufikia kiasi cha dola milioni 450.