1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Bomu lalipuka na kuuwa 13.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeY

Shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mgahawa mmoja karibu na eneo la msikiti mwekundu mjini Islamabad nchini Pakistan limesababisha vifo vya kiasi watu 13 na kuwajeruhi wengine 70.

Wengi wa wahanga wa shambulio hilo walikuwa ni maafisa wa polisi.

Bomu hilo lililipuka ndani ya hoteli moja karibu na msikiti mwekundu mjini Islamabad, baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi wa kidini ambao walikuwa wameushikilia msikiti huo wakidai kurejeshwa kwa kiongozi wao wa kidini anayependelea mahusiano na kundi la wapiganaji wa Taliban Maulana Abdul. Hapo awali serikali iliufungua msikiti huo kwa matumizi ya kawaida , wiki mbili baada ya jeshi kuuzingira na kuwaondoa wapiganaji.