1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Jaji Mkuu amshutumu Musharraf

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxv

Maelfu ya wanasheria na wanachama wa vyama vya upinzani wameandamana kumuunga mkono jaji mkuu wa Pakistan aliesimamishwa kazi na Rais Pervez Musharraf.

Iftikhar Chaudhry alikuwa akizungumza kwenye semina juu kutenganisha madaraka na uhuru wa vyombo vya mahkama. Ameuambia umma kwamba mahkama huru ni ngao madhubuti dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka na utawala wa kidikteta.

Rais Musharraf alimsimamisha kazi jaji huyo mkuu kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake miezi miwili ilopita na kupelekea kuzuka kwa maandamano ya ghasia yaliofanywa na wapinzani na wanasheria.

Mapambano kati ya wafusi wa serikali na wapinzani wiki mbili zilizopita yameuwa watu 41 mjini Karachi.