1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Jemadari Musharraf atangaza hali ya hatari

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A8

Rais wa Pakistan,Pervez Musharraf ametangaza hali ya hatari katika nchi yake.Akitetea hatua hiyo amesema,anajibu tishio la wanamgambo linalozidi kuwa kubwa na vile vile serikali inashindwa kufanya kazi kwa sababu mahakama inaingilia kati. Katiba ya nchi imeahirishwa na askari polisi wamezingira jengo la Mahakamu Kuu.Jaji Mkuu Ifitkar Chaudhry ameondoshwa kazini.Mahakama Kuu ilitazamiwa kutoa hukumu yake siku ya Jumanne juu ya uhalali wa kumteua Musharraf mwezi uliopita, kugombea tena uchaguzi wa rais huku akishika madaraka ya kijeshi.