1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Maandamano yafanyika Islamabad

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7e

Maelfu ya mawakili na wanaharakati wa kisiasa nchini Pakistan wanafanya maandamano nje ya mahakama kuu mjini Islamabad huku kesi kati ya rais Pervez Musharaf na jaji anayejaribu kumfuta kazi ikiendelea hii leo.

Rais Musharaf aliitumbukiza Pakistan katika mzozo mkubwa wa kisheria mnamo tarehe 3 mwezi uliopita wakati alipomsimamisha kazi jaji mkuu Iftikhar Chaudhry na kuamuru jopo la majaji lichunguze madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya jaji huyo.

Wakipiga kelele za kumtaka rais Musharaf ang´atuke, mawakili na watetezi waliizingira gari alimokuwa jaji Chaudhry wakali alipowasili kwenye mahakama mjini Islamabad.

Kiongozi wa upinzani, Imran Khan, amesema maandamano ya leo yanalenga kutoa ujumbe kwa mahakama kwamba haipaswi kutii amri inayotolewa na makao makuu ya jeshi la Pakistan.