1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Mkutano wajadili migogoro ya Mashariki ya Kati

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOh

Mawaziri wa masuala ya nje kutoka mataifa saba ya Kiislamu wanakutana hii leo katika mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.Wanasiasa hao wanaijadili migogoro ya Mashariki ya Kati.Syria na Iran hazikualikwa kwa sababu ya kuhusika moja kwa moja na mivutano hiyo.Mkutano wa Islamabad unafanya matayarisho ya mkutano wa kilele wa viongozi wa madola na serikali,unaotazamiwa kufanywa mjini Mekka,Saudi Arabia.Tarehe ya mkutano huo lakini bado haijapangwa.