1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Musharraf agoma kuondowa hali ya hatari

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJf

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto yuko katika mji wa Lahore kabla ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga utawala wa hali ya hatari hapo Jumanne.

Bhuttto amesema tangazo la Rais Musharraf hapo jana la kufanyika uchaguzi wa bunge hapo mwezi wa Januari ni hatua nzuri lakini amesema kutokana na kuwepo kwa utawala wa hali ya hatari itakuwa vigumu kufanya kampeni.

Musharraf hapo jana ametetea uamuzi wake wa kutangaza utawala wa hali ya hatari huku kukiwepo na shinikizo la kimataifa kuondolewa utawala huo.

Marekani mojawapo ya waungaji mkono wakuu wa Musharraf imeikaribisha hatua ya Musharraf ya kutangaza tarahe ya uchaguzi lakini waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolleezza Rice amesema kwamba utawala wa hali ya hatari lazima uondolewe nchini huno haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Jumuiya Madola wanatazamiwa kukutana baadae leo hii mjini London Uingereza kujadili iwapo au la kusitisha uwanachama wa Pakistan kwenye jumuiya hiyo ya takriban nchi nyingi ziliokuwa makoloni ya zamani ya Uingereza.