1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Pakistan yafanya jaribio la kombora

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPO

Pakistan imefanya jaribio la aina mpya ya kombora la masafa marefu. Afisa wa jeshi mjini Islamabad amesema kombora aina ya Shaheen II lililovurumihswa kutoka mahali pa siri, lililenga mahala palipotarajiwa.

Kombora hilo lina uwezo mkubwa wa kulenga mahala linapotakiwa na linaweza kuvurumisha vichwa vya nyuklia na silaha nyengine. Kombora aina ya Shaheen II linaweza kwenda umbali wa kilomita 2,000.