1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Sharif arudishwa Saudi Arabia

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBR1

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan na kiongozi wa upinzani nchini humo Nawaz Sharif amerudishwa Saudi Arabia baada ya kuwasili kwake nchini Pakistan leo hii.

Mwanasiasa huyo alikamatwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege kwa madai ya rushwa na aliondolewa uwanjani hapo kwa helikopta ya polisi kabla ya kurudishwa tena uwanjani na kuingizwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Pakistan aina ya aina ya Aibus iliondoka kueleka Jeddah.

Wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Islamabad Sharif aligoma kukabishi paspoti yake kwa maafisa wa uhamiaji. Kabla ya kuwasili Pakistan Sharif alisema alikuwa amejiandaa kwa lolote lile.

Sharif alipinduliwa na Rais Generali Pervez Musharraf katika mapinduzi ya mwaka 1999.Alikubali kwenda kuishi uhamishoni na kuachana na Pakistan kwa miaka 10 ili kuepuka hukumu ya kifo kwa madai kadhaa yakiwemo yale ya rushwa.