1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Wanasheria watimuliwa kwa marungu

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLd

Polisi wa kuzuia vurugu wametumia marungu na gesi ya kutoa machozi kutawanya mamia ya wanasheria waliokuwa wakiamandamana katika mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.Ripoti zinasema,watu darzeni kadhaa wamejeruhiwa.Machafuko hayo yametokea baada ya Halmashauri ya Uchaguzi ya Pakistan kumuidhinisha Rais Pervez Musharraf kama mgombea urais kwa awamu nyingine ya miaka mitano,wakati akibakia kiongozi wa majeshi.Makundi ya upinzani yalijaribu kwa njia ya kisheria kumzuia Musharraf kugombea urais katika mavazi ya kijeshi,lakini Mahakama Kuu imetoa idhini yake.Uchaguzi wa rais umepangwa kufanywa tarehe 6 Oktoba.