1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad : Wenye itikadi kali wampiga Iamamu aliyeteuliwa na serikali

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBem

Mamia ya wanafunzi wa kidini wamemzuwia Imamu aliyeteuliwa na serikali kuongoza ibada katika msikiti mwekundu ambako zaidi ya watu mia moja waliuwawa hivi karibuni katika mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wanaharakati wakiislamu wa itikadi kali, baada ya msikiti huo kuvamiwa .

Waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa Imamu Abdul Aziz ,anayewaunga mkono Watalibani. Abdul Azizi kwa sasa yuko gerezani.

Kadhalika walipiga kelele wakilaani hatua ya Rais Pervez Musharraf kuuvamia msikiti huo na kumuunga mkono Makamu wa Abdul Aziz, Abdul Rashid Ghazi aliyeanzisha uasi kwa kuukalia msikiti huo, hadi alipopigwa risasi na kuuwawa na majeshi ya serikali.