1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad.Bomu lalipuka karibu na ofisi ya Musharraf.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B8

Shambulio la bomu lililotegwa kando ya barabara karibu na kituo cha kijeshi ambapo anaishi rais Pervez Musharraf wa Pakistan ,. Limesababisha vifo vya kiasi watu saba na kuwajeruhi wengine wengi. Shambulio hilo lililotokea jana katika mji wa Rawalpindi kiasi cha kilomita moja kutoka makao ya rais Musharraf. Alikuwa ofisini mwake wakati wa shambulio hilo lakini hakuathirika. Hili ni shambulio la hivi karibuni kabisa katika wiki za karibuni ambalo limehusishwa na wapiganaji wa Kiislamu. Kiasi watu 140 wameuwawa mapema mwezi huu mjini Karachi wakati washambuliaji waliposhambulia magari yaliyomchukua waziri mkuu wa zamani Benazir Bhuto pamoja na wafuasi wake saa chache baada ya kurejea nchini humo baada ya miaka nane ya kuishi uhamishoni.