1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Maandamano yakupinga mashambulio dhidi ya Bhutto

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EB

Mamia ya waandamanaji wenye hasira wamefanya mikutano na kuzuia njia kwa kuwasha moto katika barabara za miji kadhaa kusini mwa Pakistan kufuatia tukio la jaribio la kutaka kumuua waziri wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto.

Waandamanaji hao wengi wakiwa vijana waliwalazimisha wafanyibiashara kufunga maduka yao katika wilaya ya Liari huko Karachi na kuwapiga mawe polisi wakupambana na fujo.

Watu watano wamejeruhiwa kufuatia ghasia hizo.

Benazir Bhutto amelayalaumu makundi kadhaa ya wanamgambo yaliyoko nchi jirani kwa mashambulio hayo.

Maafisa wa Pakistan wanashuku jaribio hilo la kumuua Bhutto lilipangwa na kiongozi wa Taliban.Hata hivyo Kiongozi huyo Kamanda Baitullah Mehsud mwenye makao yake katika jimbo tete karibu na Afghanstan amekanusha madai hayo akisema Taliban kamwe haijafikiria kumuua mtu asiye na hatia.

Licha ya hali ya mambo Bhutto leo hii anakutana na viongozi wa chama chake kupanga mikakati zaidi ya kuendeleza kampeini yake kabla ya uchaguzi.