1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Musharraf ataka kutumia jeshi kubakia madarakani.

25 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMj

Kiongozi wa kijeshi wa Pakistan jenerali Musharraf amesema ataendelea kuwa mkuu wa jeshi ikiwa hatachaguliwa tena kutumikia kipindi kingine cha urais.Mahakama kuu ya nchi imeambiwa hayo na serikali leo.

Tamko hilo linathibitisha kwamba jenerali Musharraf bado anaweza kulitumia jeshi ili kung’ang’ania madaraka ikiwa atashindwa katika uchaguzi.