1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Pakistan yaionya India

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXC

Pakistan imeonya dhidi ya hatua yoyote itakayochukuliwa na India ya kutaka kufanya jaribio la nuklia, ya kwamba hatua hiyo itaanzisha ushindani wa silaha kartika eneo la Asia.

Onyo hilo linafuatia taarifa ya kwamba Australia inapanga kuiuzia India madini ya Uranium yanayotumika katika utengenezaji wa silaha za nuklia.

Serikali ya India imesema mkataba wa ushirikiano uliyopendekezwa na Marekani juu ya uzalishaji wa nishati ya nuklia kwa matumizi ya kiraia, hauizui kuendelea na mpango wake wa silaha za nukilia ikiwa ni pamoja na majaribio ya silaha hizo.

Akizungumzia hali hiyo msemaji wa wizara ya nje ya Pakistan Tasnin Aslam alisema