1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu kufanyika mapema mwaka ujao

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Go

Uchaguzi mkuu wa nchini Pakistan unapangwa kuanyika mapema mwaka ujao.

Waziri mkuu wa Pakistan Shaukhat Aziz amesena kwamba uchaguzi huo utafanyika mapema mwezi Januari mwaka 2008.

Katika kipindi kisichopungua wiki moja rais Pervez Musharraf alijinyakulia wingi wa kura katika uchaguzi wa rais.

Rais Musharraf anasubiri kuidhinishwa rasmi na mahakama kuu.

Uchaguzi huo wa rais ulisusiwa na vyama vya upinzani.