1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISMAILIA:watu tisa wauwawa kwenye ajali ya ndege ya kikosi cha waangalizi wa kimataifa

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4K

Ndege ya kikosi cha waangalizi wa kimataifa wanaohusika na kusimamia mpaka wa Israel na Misri imeanguka katika eneo la Sinai na kuuwa watu tisa.

Duru zinasema ndege hiyo ilianguka kwenye barabara na kugonga lori ambalo liliripuka.

Miili iliyoteketea inayofikiriwa ni ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo ilipatikana kwenye mabaki ya ndege hiyo.

Duru pia zinaarifu dereva wa lori hilo aliruka kutoka kwenye lori na inaaminika amenusurika.hata hiyvo kilichosababisha ajali ya ndege hakikujulikana mara moja.

Ndege hiyo ilikuwa ina watu kiasi cha tisa wote raia wa Ufaransa.

Taarifa za kiusalama zinasema ndege hiyo ilikuwa inatokea El Gorah kaskazini mwa Sinai kuelekea Saint Catherin kusini mwa eneo hilo.