1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yahatarisha jitahada za amani Mashariki ya Kati

P.Martin/ZPR10 Januari 2011

Umoja wa Ulaya,Marekani na Wapalestina wamehamakishwa baada ya Israel kubomoa sehemu ya jengo la hoteli moja mashuhuri katika Jerusalem ya Mashariki kwa azma ya kujenga makaazi ya Wayahudi.

https://p.dw.com/p/QpI6
A construction worker works on a new housing unit in the east Jerusalem neighborhood of Har Homa, Wednesday, Dec. 8, 2010. The European Union's Jerusalem Report 2010, an annually released document that was leaked this week, said Israel's policies of construction in east Jerusalem were harming prospects of Palestinians establishing their capital there. Israel views Jerusalem as its undivided capital. Palestinians seek its eastern sections of the city for the capital of their future state. (AP Photo/Sebastian Scheiner)
Baadhi ya makaazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi katika Jerusalem ya Mashariki.Picha: AP
Palestinian President Mahmoud Abbas shakes hands with the European Union Foreign Policy Chief Catherine Ashton in the West Bank city of Ramallah, Thursday, Jan. 6, 2011. Ashton is on an official visit to the region. (AP Photo/Majdi Mohammed, Pool)
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Catherine Ashton(kushoto) pamoja na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas.Picha: AP

Wajumbe wa Kipalestina wamesema, hatua hiyo ya Israel imeondoa uwezekano wo wote ule wa kurejea katika majadiliano ya amani.Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton, ameionya Israel kuwa ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Waarabu ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.Nae waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton amesema, hatua hiyo ya Israel inahatarisha jitahada za amani katika Mashariki ya Kati.