1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaizuwia mashua ya bidha kwenda Gaza

7 Desemba 2008
https://p.dw.com/p/GB1V
Jerusalem:
Wanajeshi wa usalama wa Israel leo waliingia kwenye mashua moja katika bandari ya Jaffa kuwazuwia wabunge wa kiarabu kutuma msaada ukanda wa Gaza,wakikiuka amri ya kulifunga eneo hilo.
Mbunge mmoja wa kiarabu katika bunge la Israel Ahmed Tibi alisema, walikua wakijiandaa kupeleka madawa na mahitaji mengine muhimu katika ukanda huo wa Gaza wakati jeshi la wanamaji lilipowazuwia. Wabunge wengine wakiarabu na wanaharakati wa Kiyahudi wa siasa za mrengo wa shoto na wapigania amani walikuwemo ndani ya mashua hiyo.Israel imeimarisha hatua yake ya kulifunga eneo la Gaza tangu yalipozuka machafuko mpakani tarehe 4 mwezi uliopita, kiruhusu kungia chakula na mafuta kwa siku nne tu, katika muida wa wiki kadhaa.Wiki iliopita meli za kijeshi za Israel ziliizuwia kuwasili Gaza ,meli moja ya Libya iliokua akisafirisha tani 3.000 za bidhaa .