1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yataka kurejea mazungumzo na Syria

25 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgB

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa angependa kurejea katika mazungumzo ya amani na Syria, lakini amesisitiza kuwa kwanza Syria iache kuviunga mkondo vikundi vya Hamas na Hizbollah.

Syria hivi karibuni ilionesha nia ya kutaka kurejea katika meza ya mazungumzo na Israel.

Wakati huo huo katika hatua inayoonekana kuimarisha uhusiano na wapalestina, waziri wa ulinzi wa Israel Amir Peretz ametangaza hatua za kulegeza vikwazo dhidi ya wapalestina, katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu wapalestina wengi kwenda Israel kufanya kazi.

Serikali ya Israle pia inangalia uwezekano wa kuwaachilia wafungwa zaidi wa kipalestina kutoka katika magereza ya Israel.

Baada ya mazungumzo na rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas hapo juzi , Israel ilikubali kuachia dola millioni 100 na kuzikabidhi kwa mamlaka ya Palestina.