1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL : Aokolewa kwenye jengo lililoanguka

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6i

Mtu mmoja ametolewa akiwa hai kwenye kifusi cha jengo la ghorofa sita ambalo limeanguka mjini Istanbul Utruki hapo jana.

Mtu mwengine bado amenasa chini ya kifusi cha jengo hilo. Sababu ya kuanguka kwa jengo hilo bado haijulikani lakini kondarasi wa jengo hilo analaumiwa kwa uzembe.Gavana wa mji wa Istanbul Muammer Guler amesema takriban wakaazi wote wa jengo hilo walikuwa wametoka kwenye jengo hilo kama saa moja kabla ya kuanguka baada ya kulisikia likidata.

Inaonekana kwamba jengo hilo lilikuwa limeathirika kutokana na tetemeko la ardhi la mwaka 1999.

Shughuli duni za ujenzi nchini humo zimekuwa zikilaumiwa kwa maelfu ya vito kutokana na matetemeko ya ardhi.