1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. Jeshi bado lasisitiza kuhusu kiongozi asiyeelemea katika dini.

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdb

Kiongozi wa jeshi la Uturuki kwa mara nyingine tena amesema kuwa rais atakayeingia madarakani nchini humo ni lazima aendeleze sera za kutenga dini na utawala.

Hali hii itarejesha tena mjadala na chama tawala kinachoelemea katika dini ya Uislamu kuhusiana na mgombea wao baada ya ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni.

Uturuki ilitumbukia katika mzozo Aprili mwaka huu wakati jeshi lilipokataa uteuzi wa chama cha AKP kwa waziri wa mambo ya kigeni Abdullah Gul , mfuasi wa zamani wa chama cha Kiislamu , kuwa rais wa nchi hiyo. Mzozo huo ulileta mvutano katika nchi hiyo ambayo ina Waislamu wengi kwa maandamano dhidi ya rais huyo wa chama cha AKP, kutokana na shutuma kuwa chama cha waziri mkuu Erdogan kinataka kuielekeza serikali ya nchi hiyo isiyoegemea katika dini katika taifa zaidi la Kiislamu.