1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Merkel amekutana na Erdogan nchini Uturuki

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5i

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,amekutana naa waziri mkuu wa uturuki,Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul.Merkel ametoa wito wa kufanywa majadiliano kwa mapana na marefu,kuhusu masuala ya utamaduni na dini,kati ya Ujerumani na Uturuki.Hapo awali mjini Ankara,Kansela Merkel alisema,juhudi ya Uturuki kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya,yategemea nchi hiyo kutekeleza kwa ukamilifu masharti ya uanachama.Vile vile bidhaa za Cyprus ziruhusiwe kusafirishwa kupitia bandari na viwanja vya ndege vya Uturuki.Waziri mkuu wa Uturuki kwa upande wake,ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kwanza uondoe vikwazo vya biashara vilivyowekwa dhidi ya Cyprus ya Kituruki.Kansela Merkel aliefuatana na ujumbe wa kibiashara wa mameneja 20,leo hii anakamilisha ziara yake nchini Uturuki kwa kukutana na wanabiashara na viongozi wa dini mbali mbali.