1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Itali yaitoa Ufaransa

18 Juni 2008

Katika kombe la Ulaya ,mabingwa wa dunia Itali wameipuku tena Ufaransa kwa 2:0.

https://p.dw.com/p/EMAk
Luca Toni atamba.Picha: Reuters/Michael Kooren

Kwaheri "Les Blues"-kwa heri makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa katika kombe la Ulaya 2008.Hizo ndizo salamu za waazzuri-au-wataliana kwa wafaransa baada ya kuwazaba jana mabao 2:0.

Ufaransa imeshindwa kulipiza kisasi cha finali ya kombe la dunia 2006 nchini Ujerumani ilipopokonywa kombe la dunia na Itali.

Katika mpambano wapili jana,Holland, licha ya kuteremsha timu B,haikutoa sadaka pointi 3 kwa warumania licha ya kuwa wadachi walikwishakata tiketi yao zamani ya robo-finali.

"Adieu,les Bleus"-kwa heri Ufaransa,tenahii ni mara ya pili baada ya finali ya kombe la dunia-wataliana wanawafungisha virago jirani zao wafaransana kuwarudisha Paris,mikono mitupu.Kwa ushindi huo,Itali,mabingwa wa dunia wana miadi jumapili hii kwa changamoto ya robo-finali na jiran i zao wengine Spian.

Kwa wafaransa jana mambo yalianza kuwaendea kombo tangu dakika ya 8 ya mchezo,pale jogoo lao Franck Ribbery,lilipotiwa munda na kuumia.Ufaransa bila jogoo,haikuweza tena kuwika.kama msumari mwengine katika jeneza lao, mlinzi wao alifanya madhambi katika eneo la adhabu alimpompiga mwerteka mshambulizi hatari wa Itali Luca Toni aliekua akielekea na dimba uso kwa uso na kipa wa Ufaransa.

Mkwaju wa penalty,ukachimba zaidi kaburi la wafaransa mjini Zurich kabla nahodha wao Thiery Henry, kuupiga msumari wa mwisho katika jeneza la Ufaransa alipousindikiza mkwaju wa free-kick kimiyani mwa lango lake.

Kwa kweli,haikua siku njema kwa wafaransa na wataliana ambao waliokolewa kubakia mashindanoni na kipa wao aliozima mkwaju wa penalty katika mechi na Rumania,bahati ni yao.

Kocha wa Ufaransa Raymond Dominique anajua kwamba mashabiki wa Ufaransa sasa wameshanoa shoka lao na wanataka kichwa chake.Yeye hakufurahishwa na uamuzi wa rifu wa kumtimua mlinzi wake:

"Nafikiri haukua uamuzi wa busara kumtimua nje.Nahisi kuna maamuzi yaliopitishwa jana yaliopelekea mchezo wetu kuparaganyika na hasa katika kipindi cha kwanza."

Ufaransa ikifunga leo virago na kuvuka mpaka wa Uswisi kurudi nyumbani na pengine kuunda timu mpya chini ya kocha mpya, Holland iliudhihirishia ulimwengu wa dimba kuwa wao wanaelewa "fair play"-mchezo bila maonevu.Ingawa waliteremsha timu B, hatahivyo, waliondoka na pointi 3 ambazo hawakuhitaji kuingia duru ijayo.

Baada ya kuicharaza Itali mabao 3-0 na Ufaransa 4-1, Holland jana ilikamilisha ushindi wa 3 ilipoibwaga Rumania mabao 2:0.

Sasa ina miadi jumamosi hii ama na Sweden au Russia zinazocheza jioni hii.Stadi wao mmoja akiulizwa kwanini hawakuiachia Rumania ushindi wa bure na kuzitoa nje Itali na Ufaransa, alijibu:

"Tumejipatia pointi 3 kwa kutokwa na jasho.Kwahivyo,tunahisi haifai kuigaia timu yoyote pointi 3 za bure ."

Leo Sweden na Urusi -mojawapo itakamilisha robo-finali ya mwisho .Changamoto ya pili leo ni kati ya mabingwa waliovuliwa taji Ugiriki na Spian,yenye miadi ya robo-finali jumapili hii ijayo na mabingwa wa dunia-Itali.