1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia na Brazil kuumana katika dimba la wanawake

Sekione Kitojo
18 Juni 2019

Italia ambayo imekuwa timu iliyoleta  mshangao mkubwa  katika mashindano  haya  ya  fainali  za  kombe  la  dunia  kwa  wanawake inalenga  kuiga mfano  wa  Ujerumani  na  Ufaransa  kwa  kuwa vinara wa makundi yao.

https://p.dw.com/p/3KeOJ
FIFA Frauenfußball WM 2019 Brasilien - Australien
kikosi cha BrazilPicha: Getty Images/AFP/G. Julien

Hali hiyo itajitokeza  wakati  itakapokumbana  na  Brazil katika mpambano  ambao unarejesha kumbukumbu  za  zamani  za kombe la  dunia kwa  wanaume. Nigeria ilifungwa  bao 1-0 na  Ufaransa,  lakini ikiwa  katika nafasi  ya  tatu  katika  kundi  lao  A  inasubiri  kuona iwapo inaweza kupenya  katika timu 16 zinazosalia  ili  kuingia  katika  awamu  ya mtoano. 

Fussball  FIFA Frauen WM Australien - Italien
Wachezaji wa Italia wakishangiria bao dhidi ya AustraliaPicha: picture-alliance/AP Photo/F. Seco

Italia  ina  pointi sita baada  ya  kufunga  mabao  saba  katika michezo  yake  miwili  ya  ufunguzi , ikiwa  ni  pamoja  na  ushindi  wa kushitua dhidi  ya  timu  iliyopigiwa  upatu  kufanya  vizuri  kabla  ya mashindano  hayo Australiam, na  inahitaji  sare tu  dhidi  ya  Brazil kujihakikishia  kuwa  vinara  wa  kundi C.

Pambano  hiyo linazusha  kumbukumbu  ya  fainali  za  wanaume katika  kombe  la  dunia, ikiwa  ni  pamoja  na  kichapo kilichotayarishwa  kupitia  Pele enzi  hizo  cha  mabao 4-1 dhidi  ya Italia  katika  fainali  ya  mwaka  1970  na  mabao  matatu  ya  Paolo Rossi mwaka  1981, ambayo  yalikizamisha  kikosi  kilichokuwa kinaongozwa  na  Zico  na  hatimaye Italia  kutoroka  na  taji  hilo.

Australia  inaweza  kunyakua  nafasi  ya  pili iwapo  wataishinda Jamaica, ambao  wameshindwa  kupata  bao  wakati  wakipoteza michezo  yao  yote, na  Brazil  kushindwa  kupata ushindi.

FIFA Frauenfußball WM 2019 Brasilien -Jamaika Fans
Shabiki wa JamaicaPicha: Getty Images/Elsa

Ufaransa vinara kundi A

Norway  inawasubiri  viongozi  wa  kundi  C katika  awamu  ya  timu 16 zitakazobaki  baada  ya  kikosi  cha  kocha  Martin Sjogren kuwapiku Korea  kusini  kwa  mabao 2-1 mjini  Reims jana  Jumatatu, na  kumaliza wapili  katika  kundi A.

Ufaransa  imejihakikishia  kuwa vinara wa  kundi A baada  ya  kupata bao moja  tu  katika  mchezo  wake  dhidi  ya  Nigeria, bao lililofungwa  kutokana  na  mkwaju  wa  penalti ambayo  ilibidi kurudiwa  mjini Rennes.

Ufaransa  inakabiliwa  na  uwezekano  wa  pambano  la  robo fainali dhidi  ya  mabingwa  watetezi Marekani  iwapo Marekani  itakuwa vinara  wa  kundi F na  kuingia  katika  timu 16 kama  inavyotarajiwa.

FIFA Frauen-WM 2019 | Deutschland vs. Südafrika | 4. TOR Deutschland
Wachezaji wa Ujerumani sare nyeupe wakishangiria bao dhidi ya Afrika kusiniPicha: Reuters/J.P. Pelissier

Ujerumani  imehakikisha  kwamba  inaikwepa  Marekani  katika awamu  ijayo  baada  ya  kuirarua  Afrika  kusini  kwa  mabao 4-0 na kumaliza  ikiwa  kileleni mwa  kundi B.

Uhispania  inauwezekano  wa  kutiana  kifuani  an  Marekani  baada ya  kumaliza  ikiwa  ya  pili  katika  kundi B nyuma  ya  Ujerumani baada  ya  kutoka  sare  bila  kufungana  na  China ambao  pia wanahakika  ya  kuendelea  na  mashindano  hayo  kama  timu bora ya  tatu.