1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ivory Coast

27 Novemba 2010

Uchaguzi nchini Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/QJkS
Aliyekuwa waziri mkuu wa Ivory Coast, Alassane Ouattara katika kampeni za uchaguzi.Picha: Picture alliance/dpa

Wapinzani wakisiasa nchini Ivory Coast hapo jana walikamilisha mikutano ya kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo kesho na ambao unatarajiwa kumaliza mwongo mmoja wa kutoimarika kwa nchi hiyo inayogubikwa na hofu na umwagikaji damu.

Maelfu ya wafuasi walimiminika katika mikutano tofauti ya rais Laurent Gbabo na mpinzani wake Alassane Outtara katika mji mkuu wa  kibiashara wa Abidjan, ambao ni eneo kuu la upigaji kura katika nchi hiyo iliyogawanyika.

Präsidentschaftswahlen Elfenbeinküste Laurent Gbagbo
Rais Laurent Gbagbo, akiwasili katika kampeni.Picha: picture alliance/PANAPRESS/MAXPPP

Wagombea wa uchaguzi huo wametoa wito wa kupigwa kura kwa amani, lakini dalili za vurugu  zilionekana wakati kambi ya Outtara ilipokataa wito wa Gbabo wa kuwepo amri ya kutotembea baada ya uchaguzi wa kesho. Vikosi vya jeshi nchini humo na vya Umoja wa Mataifa  vimemiminika kuimarisha usalama iwapo patazuka vurugu.

Mwandishi :Maryam Abdalla/Afpe

Mhariri:Sekione Kitojo