1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J2 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRp

Sydney . Viongozi wakubaliana kupunguza gesi zinazoharibu mazingira.

Viongozi 21 wanaokutana katika mkutano wa ushirikiano baina ya mataifa ya Asia na yale yanayopakana na bahari ya Pacific mjini Sydney wametia saini makubaliano yenye lengo la kupunguza ujoto duniani.

Waraka huo wa makubaliano unatoa wito wa hatua za muda mrefu za kupunguza gesi zinazoharibu mazingira.

Miongoni mwa mambo mengine, unatoa wito pia wa upunguzaji wa matumizi makubwa ya nishati, ama kiasi cha nishati inayohitajika katika ukuaji wa uchumi, kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo haya na malengo mengi mengine ambayo yamo katika waraka huo wa makubaliano hayailazimishi nchi yoyote kuyatekeleza.

Mwenyeji wa mkutano huo waziri mkuu wa Australia John Howard, amesema kuwa makubaliano yanaonyesha nia thabiti ya kundi hilo la mataifa kuangalia athari za ujoto duniani ikiwa wakati huo huo ukitoa nafasi kwa ajili ya ukuaji wa uchumi.