1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Idadi ya vifo yaongezeka

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLh

Idadi ya vifo vya watu waliouwawa kufuatia tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia imeongezeka na kufikia watu kiasi ya 70. Mamia ya watu walijeruhiwa kwenye tetemeko hilo la kipimo cha 6.3 kwenye vipimo vya Richter.

Katika mji wa Padang, mji mkuu wa jimbo la Sumatra Magharibi, tetemeko hilo limezusha hofu miongoni mwa wakaazi wakifikiri huenda likazusha tsunami. Kiongozi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa mjini Padang, Ayu Purwaningsih amesema, ´Tetemeko la ardhi limezusha hofu hususan katika miji ya Batusangkar, Solok, Bukittingi na Padang. Mjini Pandan watu wengi wanahofia tusanami. Watu wamezikimbia nyumba zao, watoto wa shule wakapiga mayowe na hata hospitalini kukawa na mtafaruku. Baadaye tulitangaza hakuna onyo la kuzuka tusanami ndio watu wakatulia.´

Duru za polisi zinasema majengo mengi yameporomoka na idadi ya vifo huenda ikaendelea kuongezeka huku juhudi za uokozi zikiendelea.

Tetemeko hilo limeyatikisa maeneo ya nchini Malaysia na Singapore ambako watu wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao.