1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Jiji lakumbwa na tetemeko la ardhi

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBax

Tetemeko la ardhi la kiwango cha vipimo vya rishta 7.5 limeutikisa mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia.

Majumba marefu yalitikisika kwa kishindo na kusababisha hali ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi waliokimbia huku na kule katika barabara za mji wa Jakarta.

Hakuna taarifa yoyote ya majeruhi au hasara kufuatia tetemeko hilo.

Tetemeko hilo lilituwama kwa umbali wa kilomita 100 mashariki mwa mji wa Jakarta.

Watalaamu wa jiolojia wamesema kwamba hakuna hatari ya wimbi la Tsunami kutokana na nguvu za tetemeko hilo.