1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamadari Petraues na vita vya Irak

9 Aprili 2008

Amirijeshi mkuu wa majeshi ya Marekani huko Irak ahojiwa na Baraza la Senat la Marekani jinsi vita vinavyoenda.

https://p.dw.com/p/Dexh

Maendeleo yamefanyika,lakini vikosi vya Marekani bado vitaendelea kuhitajika nchini Irak.Hiyo ndio risala muhimu aliotoa jana Jamadari David Petraeus -amirijeshi mkuu wa Marekani nchini Irak mbele ya Baraza la senat la Marekani,huko Washington.

►◄

Mara kwa mara ,jamadari Petraeus akikumbusha :vita nchini Irak havitaleta ushindi kwa kutumia nguvu tu za kijeshi,lakini juu ya hivyo, rais George Bush aliamua kiasi cha mwaka mmoja uliopita kuendelea kuongeza majeshi na kutumia turufu ya nguvu kushinda vita hivyo.

Wakatumwa askari 20,000 zaidi ili kuleta nafuu katika safu mbali mbali za vita.matumizi ya nguvu yakapungua -hujuma si nyingi hivyo kama ilivyokua n a ni maafa machache ya waliofariki kuliko kabla ya kutumwa majeshi hayo zaidi.

Licha ya hayo, hali ya mambo -miaka 5 tangu kuanza vita, Irak ingali katika msukosuko na machafuko wala haijatulia.Kwa jinsi isivyotulia, tangu jamadari Petraeus hata balozi wa Marekani mjini Baghdad Crocker ,wanaonya kutorejesha nyumbani wanajeshi zaidi.

Ni mara ya pili hii wanabidi kuitetea siasa ya kamanda wao mkuu-rais Bush-mbele ya Bunge la Marekani na kwa wamarekani.Wanajitahidi sana lakini ,hawahisi wanafaulu kuwasadikisha.

Matamshi yao yanalingana na yale waliotoa miezi 7 iliopita. Kuna maendeleo ,lakini hayatoshi na yanaregarega.

Mara kwa mara swali la kimsingi linaulizwa: Tena hata na watetezi 2 wa kiti cha urais -seneta Hilary Clinton na Barack Obama.Kifanyike nini nchini Irak ili wanajeshi waweze kurejeshwa nyumbani tena mambo yakiwa mazuri au mabaya.

Lini mtu aweza kusema kuna mafanikio nchini Irak ?Lini hali itakua si ya kuvumilika tena kmumbidi rais kuamrisha majeshi yafunge virago na kuihama Irak ?

Si jamadari Petraeus wala balozi Crocker waweza kujibu ,kwani hakuna kipimo serikalini cha kupitisha uamuzi huo.

Rais Bush ameripua vita hivi akitumia mkakati uliopotoka na hayuko tayari kujifunza kutoka makosa aliotenda.

Alichobakiwa nacho ni subirini tu mambo yatatengenea wenyewe na kutegemea majeshi kufumbua kitandawili.

Lakini njia hiyo haifumbui kitandawili cha Irak na tangu wanajeshi wa Marekani hata wenzao wa ki-iraqi wanatoa mhanga kwa uongozi potofu wa vita hivi.Hadi sasa wanajeshi 4000 wa Marekani wameuwawa.

Na tangu rais Bush kuimarisha vikosi zaidi,wanajeshi 100 wake kwa waume wamepoteza maisha yao nchini Irak."hawakufa bure"-ndio usemi wanaotumia wanaoungamkono vita kuendelea.Ukweli ni kuwa, mkakati mbovu hautatengeza mambo endapo ukiungan'gania.Kwani, ukiwa umepotea njia ndio umepotea.

Kwahivyo, wamarekani wamesaliwa na njia moja tu ya kufuata:tena wakiwa wanataka kitu kipya: Wanapaswa katika uchaguzi wa rais Novemba mwaka huu wamchague mtetezi wa rais kutoka chama cha democrat ama Barack Obama au bibi Hilary Clinton.Kwani kumchagua mrepublican,John McCain ni kuseleleza msimamo ule ule wa George Bush.