1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Afrika kati yajadiliwa Ndjamena

3 Aprili 2013

Viongozi wa mataifa ya Afrika kati wanakutana mjini Ndjamena,mji mkuu wa Tchad kuzungumzia mzozo wa jamhuri ya Afrika kati ambako waasi wa Seleka wamempindua rais na kusitisha katiba.

https://p.dw.com/p/188cs
Kitambulisho cha mji mkuu wa jamhuri ya Afrika kati-BanguiPicha: DW/Leclerc

Mkutano wa kille wa vongozi wa mataifa ya jumuia ya uchumi ya Afrika kati ECCAS unaofanyika mjini Ndjamena una uzito mkubwa kwa jamhuri ya Afrika kati,siku kumi baada ya mapinduzi yaliyomtimua madarakani rais Francois Bozizé.

Mkutano huu hauitishwi hivi hivi tu katika mji mkuu wa Tchad, Ndjamena.Tangu siku kadhaa sasa mchango wa Tchad katika kuporomoshwa madarakani rais wa zamani Francois Bozizé,march 24 iliyopita unazidi kubainika.Mwenyewe Francois Bozizé anaesemekana ameomba kinga ya ukimbizi nchini Benin,ameilaumu Tchad kwa "kumuacha mkono"."Vikosi maalum vya jeshi la Tchad ndivyo vilivyoongoza opereshini March 24 iliyopita na baadae kukishambulia kituo cha kijeshi cha Afrika kusini" amesema rais huyo wa zamani wa Jamhuri ya Afrika kati-Fracois Bozizé.

Vipi utawala wa sasa unaweza kuhalalika

Zentralafrikanische Republik Michel Djotodia
Kiongozi wa waasi wa Seleka Michel DjotodiaPicha: Getty Images

Mkutano huo wa kilele unatarajiwa kuzungumzia uwezekano wa kutumika katiba itakayoweza kuhalalisha utawala mpya wa mjini Bangui ambao hautambuliwi na jumuia ya kimataifa.Fikra moja wapo ni kuifanyia badhi ya marekebisho katiba iliyositishwa hapo awali na kiongozi mpya wa jamhuri ya Afrika kati Michel Djotodia .

Djotodia hatarajiwi kushiriki mkutanoni,kinyume na waziri mkuu Nicolas Tiangaye,wakili ambae ni miongoni mwa wapinzani wa utawala wa zamani wa Bozizé-mwanasiasa pekee anaethaminiwa na kutajwa kuwa "halali na jumuia ya kimtaifa .

Mada nyengine tete mazungumzoni inahusu mchango wa kijeshi wa Afrika kusini katika jamhuri ya Afrika kati.

Afrika kusini iliyopoteza wanajeshi wake 13 katika mapigano ya mjini Bangui inawakilishwa na rais Jacob Zuma aliyefuatana na mawaziri wake watatu-waziri wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano,waziri wa ulinzi na waziri wa usalama wa taifa.

Mkataba wa ulinzi kati ya Bozizé na Jacob Zuma

Südafrika Trauerfeier für getötete Soldaten in der Zentralafrikanischen Republik
Familia za wanajeshi wa Afrika kusini waliouliwa mjini Bangui zinaomboleza,maiti za wanajeshi hao zilipowasili PretoriaPicha: AFP/Getty Images

Duru za karibu na rais na idara za usalama nchini Afrika kusini zinasema rais Jacob Zuma alitiliana saini pamoja na Francois Bozizé "mikataba ya ulinzi" na hifadhi " mikataba inayoyapatia njia makampuni ya Afrika kusini kufaidika na utajiri wa mafuta,almasi na maadini mengine ya thamani katika majimbo mawili ya nchi hiyo,na badala yake Afrika kusini ilitakiwa iulinde utawala wa Bozizé.

Seleka wanasema mikataba hiyo haina faida yoyote kwa jamhuri ya Afrika kati na kwa hivyo wanajeshi wa Afrika kusini lazma wajeree nyumbani.

Kiroja lakini ni kwamba mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika iliyoisitishia uwanachama jamhuri ya Afrika kati,si mwengine isipokuwa Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika kusini-mke wa zamani wa rais Jacob Zuma.

Mwandishi:Hamido Oummilkheir/AFP/dpa

Mhariri: Josephat Charo