1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaribio la kigaidi, Ulaya

29 Septemba 2010

Magaidi walenga kuushambulia mji wa London, pomoja na miji mikuu nchini Ujerumani na Ufaransa.

https://p.dw.com/p/PPLh
Jaribio la kigaidi katika nchi tatu, Ulaya lagunduliwa.Picha: AP

LONDON

Mashirika ya upelelezi yamezima jaribio la mashambulizi ya kigaidi yaliyopangwa kufanyika wakati mmoja, nchini Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Taarifa hii ilitolewa na shirika la habari la Uingereza Sky. Shirika hilo la habari lilisema taarifa yake inatokana na vyanzo vya habari vya upelelezi na kwamba mpango huo wa ugaidi ulikuwa na chimbuko lake Pakistan. Mashambulizi hayo yalipangwa kufanyika wakati mmoja mjini London na katika miji mikubwa ya Ujerumani na Ufaransa. Mpango wa kufanyika kwa mashambulizi hayo unasemekana ulikuwa katika awamu za mwisho. Shirika hilo la habari la Sky, lilisema mpango huo wa ugaidi, uligunduliwa baada ya nchi hizo tatu za Ulaya kushirikiana na Marekani katika kubadilishana taarifa za upelelezi. Hapo jana watu waliondolewa katika Mnara wa Eiffel mjini Paris Ufaransa baada ya ripoti za kuwepo kitisho cha bomu.