1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Algeria itatamba kundi C ?

8 Juni 2010

Algeria yarudi Kombe la dunia tangu Mexico,1986

https://p.dw.com/p/NlQQ
Kombe la dunia: 2010

ALGERIA KATIKA KOMBE LA DUNIA:

Baada ya kipindi cha miaka 24,Algeria,inarudi katika kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini.Mara ya mwisho kucheza, ilikuwa 1986 huko Mexico.Kinyume na ilivyoshiriki mara ya kwanza na kugonga vichwa vya habari 1982 nchini Spian, kwa kuitimua Ujerumani kwa mabao 2-1 , Algeria,ilitoweka katika dimba la Afrika hadi Novemba, mwaka jana, pale ilipoipiga kumbo Misri,mabingwa wa Afrika mjini Khartoum , nje ya kombe la dunia na kukata tiketi yao ya Afrika Kusini.

Wakiwa wamefika nusu-finali ya Kombe la Afrika la mataifa mapema mwaka huu nchini Angola,mbwa mwitu wa jangwani wanatamba kwa mapana na marefu kwamba ni wao walionguruma m bele ya mabingwa wa Afrika-mafiraouni Misri.Ni wao waliowafungisha virago baada ya duru 3,Algiers,Cairo na Khartoum.

Ilikuwa Algeria pia iliowatimua Tembo wa Corte d'Iviore nje ya nusu-finali ya Kombe la Afrika kwa bao lao la dakika ya mwisho.

Hatahivyo, waafrika hawa wa kaskazini walioingia katika ramani ya dimba ya dunia pale Lekhdar Balloumi, alipotia bao la ushindi (2:1) 1982 dhidi ya Ujerumani, inaelewa ni Uingereza, ndio itakayo wanyima nafasi ya kwanza katika kundi lao C.Maadui wengine, ni Marekani na Slovenia.Hawa wawili, inatumai Algeria, kuwapikua na kuifuata Uingereza duru ya pili.

Kuna wanao dai kuwa ,Algeria, ndio timu hafifu kabisa kati ya zote 6 za Afrika. Usiidharau timu kama Algeria au Marekani.Kwani, si Marekani, iliomo kundi hili iliowatoa mabingwa wa ulaya-Spain nje ya nusu-finali ya Kombe la mashirikisho-Confederations Cup,huko huko Afrika Kusini, 2008 na kuingia finali na Brazil ?

Algeria , itamtegemea tena stadi wake ,mlinzi wa kati wa Glasgow Rangers,Madjid Bougherra, alietamba katika Kombe la Afrika nchini Angola,pale Algeria ilipomaliza nafassi ya 4 nyuma ya Misri,Ghana na Nigeria.Alikuwa Bougherra, alielifumania lango la Ivory Coast kusawazisha kabla hawakuipiga kumbo kabisa Corte d'Iviore huko Angola.Alikuwa pia ufunguo wa ushindi wa Algeria mbele ya Misri mjini Khartoum.Stadi mwengine wanae mtegemea Algeria, ni Faouzi Chaouchi, aliefungiwa hadi mpambano na Marekani.

Ngome ya Algeria, ni mabeki 4 mshahara:Antar Yahia,Rafik Halliche,Bougherra mwenyewe na Nadir Belhadj,wakati nahodha wao Yazid Mansouri na Hassan Yebda, ndio watakaotamba kama wachezaji wa kiungo kati ya uwanja.

Algeria,lakini, ina mtihani mmoja: Nani atakaeongoza mashambulio usoni ? Kocha Saadane, anaumia hapo kichwa,kwani ,Algeria, ilitia mabao 4 tu hadi nusu-finali katika kombe la Afrika.Na mabao 3 kati ya hayo 4, yalikuja katika ile changamoto na Corte d'Iviore iliorefushwa mchezo.

Mikuki ya akina Abdelkader Ghezzal,Rafik Djebbour , mkongwe Rafik Saifi pamoja na Chadli Amri,yatazamiwa kutikisa nyavu kwa Algeria.Algeria lazima iifunge Marekani, ikiwa iweke hayi matumaini ya kuifuata Uingereza duru ya pili.Tunaitakia kila heri.

Mwandishi: Ramadhan Ali/AFPE

Mhariri:Abdul-Rahman