1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je kutakuwa na mparaganyiko wa usafiri?

9 Juni 2014

Fainali za kombe la dunia zinakaribia kuanza hapo Alhamis wiki hii, huku kukiwa na mchanganyiko usiokuwa wa kawaida wa hali yenye utata kwa wenyeji Brazil na shirikisho linaloendesha mchezo huo FIFA.

https://p.dw.com/p/1CEm8
Streik in Sao Paolo Brasilien
Mgomo wa wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi mjini Sao PauloPicha: AFP/Getty Images

Majira ya baridi mjini Rio de Janeiro huambatana na hali isiyotabirika, kuna baadhi ya siku jua ni kali na unyevunyevu wenye joto kali, katika wakati wa kuelekea ufunguzi wa michezo ya fainali za kombe la dunia , ambalo linaweza kuwa , kimbunga kikali, cha kisiasa, kijamii na wasi wasi katika soka, ingawa huenda ni Brazil pekee inayoweza kuizusha hali hiyo.

Uwanja wa Maracana , utakaotumika kwa fainali ya Julai 13, ni mahali sahihi kwa ajili ya maadili na mabadiliko ya fainali hizi nchini Brazil.

Wakati jioni ikiingia , uwanja huo hung'ara kwa taa za rangi ya kijani na njano katika paa lake, wakati jua likichomoza , eneo hilo linalozunguka uwanja huo huonekana limepooza na lisilokuwa na maana, likiwa na wafanyakazi 20 tu wakishughulika kufunga nyaya za umeme katika mtaa.

Fußball WM 2014 Brasilien Stadien Rio Maracana Stadion
Uwanja wa MarakanaPicha: picture-alliance/dpa

Brazil sio nchi ya "mambumbumbu"

Brazil sio nchi kwa ajili ya watu wasiojua kitu, amesema mtunzi na mwimbaji maheremu Tom Jobim, mmoja kati ya vitu vya kufikirika katika nchi hiyo kubwa katika America ya kusini.

Jobim huenda angesema pia kuwa Brazil sio nchi kwa ajili ya Waswisi , kwasababu moja kati ya matatizo ya kombe la dunia ni tofauti za kitamaduni kati ya wataalamu na FIFA yenye makao yake makuu nchini Uswisi na nchi ambayo , kwa kusema kweli, inafanya shughuli zake tofauti kabisa.

Iwapo FIFA iliweza kuchukua kombe la dunia lililofanyika nchini Afrika kusini mwaka 2010 na kuwa watayarishaji wa fainali hizo, ambazo zilikuwa bora zaidi kuliko walivyotarajia watu wengi kutoka bara la Ulaya , hii ni kutokana na kwamba Watu wa Afrika kusini waliridhika tu na kuwa wenyeji wa kombe la dunia katika bara la Afrika.

Walijisikia kwamba hawahitaji mambo zaidi, waliishukuru FIFA.

Dilma Rousseff posiert für einen Selfie
Rais Dilma Rousseff wa Brazil akikagua ujenzi wa viwanja.Picha: DW/Marina Estarque

Hata hivyo , Brazil ni tofauti, kwa sababu ya historia yake na kujisia fahari , pamoja na nguvu kubwa za kiuchumi licha ya hali ya mparaganyiko iliyopo. Brazil haihisi kuishukuru FIFA kabisa. Kuanzia rais Dilma Rousseff hadi chini, Wabrazil wanahisi kwamba FIFA inapaswa kutoa shukrani kwa Brazil, kwa kuzileta fainali hizo kwa kile kinachojulikana kama " taifa la soka".

Kwa hiyo hamasa ni kubwa , isiyotabirika na bila kuwa na hakika ya mwisho wake.

Mgomo watishia kuleta mparaganyiko katika usafiri

Wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi mjini Sao Paulo wamekaidi uamuzi wa mahakama jana Jumapili na wanaendelea na mgomo wao unaotishia kusababisha mtafaruku katika usafiri wakati wa mchezo wa ufunguzi mjini humo ambapo Brazil itapambana na Croatia.

Wafanyakazi hao wamepiga kura kuendelea na mgomo wao saa kadhaa baada ya mahakama ya kazi kuamua kuwa ni kinyume na sheria na kuwatoza faini ya dola 222,000 kwa kila siku watakayoshindwa kuripoti kazini.

Mgomo huo umekwisha sababisha misururu mirefu ya magari katika mji huo wenye wakaazi milioni 20 wakati uwanja mpya wa mji huo unajitayarisha kuwapokea mashabiki 60,000 katika mchezo huo wa ufunguzi siku ya Alhamis.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe

Mhariri: Josephat Charo