1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je.Israel inakiuka sheria za kimataifa ?

14 Januari 2009

Israel inatumia mabomu marufuku ya phospherous Gaza ?

https://p.dw.com/p/GYGY
Vita :GazaPicha: picture-alliance/ dpa

Ushahidi unaongezeka kuwa jeshi la Israel linatumia mabomu ya "phosorous" katika hujuma zake Mwambao wa Gaza. Je,kutumia mabomu ya aina hiyo ni kukiuka sheria za kimataifa ?

Wanasiasa wa Israel na usoni kabisa waziri wa nje Zipi Livni,wamekuwa wakihakikisha tangu mwanzo wa hujuma za Israel huko gaza kwamba, juhudi kubwa zinachukuliwa kuepusha kuwadhuru huko na kuwalinda raia .Sasa wakidhurika,basi huwa yasikitisha,lakini vitani huwezi kuondosha uwezekano huo.Au wanasiasa hao wakitoa hoja kwamba chama cha Hamas kinawatumia raia kama ngano na kuwa hawawajali raia wa Israel.

Idadi inayoongezeka kila kukicha ya raia waliouwawa na waliojeruhiwa huko Gaza tangu vita hivi vilipoanza inatoa sura nyengine kabisa:Hata shirika la ukozi linalowahudumia wakimbizi huko Gaza -UNRWA hadi Chama cha Msalaba Mwekundu Ulimwenguni yanaituhumu Israel kuwa haijali raia.

Chama kinachotetea haki za binadamu cha "Human Rights Watch" kinakwenda hata mbali zaidi katika tuhuma zake: Kinaituhumu Israel katika kutumia mabomu ya "phoshereous" huko gaza ingawa ingawa hii inahatarisha raia katika eneo lililoshehni wakaazi mno kama Gaza.

Haya ni mabomu ya aina ya "phospherous" ambayo yanasababisha majaraha makubwa ya kuunguza ngozi ya mwanadamu na kwa sehemu kubwa huongoza katika kifo cha maumivu makubwa.Majeruhi wenye majaraha ya aina hiyo kwa muujibu wa madaktari huko Gaza wamewasilishwa mahospitali .-

Vikundi mbali mbali vya wapinzani katika vita hivi vimeituhumu Israel kuwa imeshafanya uhalifu wa vita.Na haikukawia kufuatia tuhuma za shirika la "human Rights watch" kuchomoza katika vyombo vya habari wakuu wa serikali ya Israel,walijaribu kwanza kunyamaa kimya na kutojibu mashtaka.

Msemaji wa wizara ya nje ya Israel alimsukumia jukumu la majibu msemaji wa Jeshi la Israel Bibi Avital Leibovich:

"Jeshi la Israel linatumia silaha kulinga na sheria za kimataifa.Hatusemi kwa urefu aina gani ya silaha tunazotumia kama tusivyosema jinsi tunavyoendesha vita vyetu.Na naweza kuwahikikishia kuwa Israel haiendi kinyume na sheria za kimataifa."

Hicho ni kielezo kisichoridhisha ingawa kisheria ni vigumu kukipinga.Sheria ya kimataifa imekataza matumizi ya mabomu ya phosherous ingawa sio moja kwa moja.yaweza kutumika kuungza,lakini sio katika maeneo yanayokaliwa na raia.

Bibi Dominique Loye, ni makamo-mwenyekiti wa Idara inayohusika na silaha katika Chama cha Msalaba Mwekundu Ulimwenguni mjini Geneva.Anafafanua mkanganyo uliopo katika sheria hii:

"Inategemea iwapo nchi fulani imetia saini mkataba huo, kwa mfano, kuna mapatano maalumu juu ya matumizi ya silaha zinazounguza moto.Ikiwa nchi fulani ,haikutia saini mapatano hayo,basi inakuwa haiwajibiki kuyaheshimu.Ikiwa nchi inasema inayaheshimu mapatano jumla ya kimataifa,inampasa mtu kuangalia ni mapatano gani hasa nchi hiyo imetia saini na iwapo nchi hiyo, inafuata sheria jumla za kimataifa na inaziheshimu."

Kuhusu mabomu ya phospherous desturi huwa hivi: Mabomu haya yakitum,ika kwa m adhumuni yakuunguza moto,jeshi lenye kufanyxa hivyo linapaswa kuchukua hadhari kuwa raia hawadhuriwi.